Ujerumani yafanya kikao cha dharura kuhusu Libya | Matukio ya Afrika | DW | 18.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Ujerumani yafanya kikao cha dharura kuhusu Libya

Kiasi ya watu mia mbili na wa tano wameuwawa huku mia tisa wakijeruhiwa katika mapambano ya wiki mbili yanayoendelea karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Serikali ya Ujerumani imeitisha mkutano wa dharura hii leo mchana wa baraza la Umoja wa Usalama kujadili hatua za kuchukuliwa katika vita vinayoendelea nchini humo baada ya bodi ya watu kumi na tano kushindwa kufikia muafaka wa makubaliano ya pamoja ya kuweka chini silaha.

Hapo jana Jumatano bodi hiyo ya watu kumi na tano iligawanyika juu ya jinsi ya kuushughulikia mzozo wa Libya na kukosa kufikia muafaka katika rasimu iliyokuwa inatoa muongozo wa namna ya kusitisha vita hivyo baina ya jeshi la Libya, LNA, na serikali ya makubaliano ya kitaifa iliyoko Tripoli, GNA.

Duru zilieleza kwamba taifa la Equatorial Guinea lilipinga rasimu iliyopendekezwa na Uingereza nayo Urusi ilikuwa makini katika mazungumzo yake ili kuepuka kumtaja Haftar kwamba jeshi lake ndilo linaloshambulia Tripoli na vile vile kudai kwamba rasimu hiyo ya Uingereza imetumia manaeno makali dhidi ya Haftar.

Ghassan Salame

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Tripoli, Ghassan Salame

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Tripoli, Ghassan Salame alitaka mapigano hayo yasitishwe mara moja kwa usalama wa raia milioni 3 wanaosihi mjini Tripoli. Kauli yake imejiri saa chache baada ya mizinga kufyetuliwa usiku wa Jumanne katika kijiji kimoja kilichoko katika wilaya ya Abu Salimu kusini mwa Tripoli.

Waziri anamfanaisha Haftar na Adolf Hitler

Waziri wa usalama wa ndani wa serikali ya Tripoli Fathi Bashagha anamshutumu Khalifa Haftar kwa mauaji yanayoendelea.

"Huu ni uhalifu wa kivita na huyu Khalifa Haftar nimwendawazimu ni Field Marshal. Huwezi kuaminii kwamma anaweza kuua watu wake namna hii. Kulipua mizinga Tripoli na unajua kuna watu wengi hapa, zaidi ya milioni tatu. Huyu ana wazimu ni zaidi ya Adolf Hitler," alisema Fathi.

Auseinandersetzungen zwischen Haftars Streitkräften und der libyschen Regierung in Tripolis

Kifaru cha jeshi la LNA

Wananchi nchini Libya wanasema wamevunjwa moyo na jumuiya ya kimataifa na baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa sababu waliwatarajia watachukua hatua za kisawa sawa kuwasimamisha wauaji na ouvu unaoendelea.

Baadaye hii leo Ujerumani ambayo kwa sasa ndio kiongozi wa baraza la Usalama itatoa mapendekezo yake baada ya kusikiliza taarifa mbali mbali kuhusiana na hali inavyoendelea nchini Libya.

Haftar amekuwa akiungwa mkno na Misri, Umoaj wa nchi za Kiarabu na Saudia na kwa kiasi fulani Urusi na Ufaransa.

(AFPE/DPAE)