1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhuru Kenyatta achaguliwa tena kuiongoza Kenya

Josephat Charo Nyiro11 Agosti 2017

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya, IEBC, Wafula Chebukati amemtangaza Uhuru Kenyatta mshindi wa uchaguzi wa 08.08.2017 kwa kupata kura 8,203,290 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Raila Amolo Odinga, aliyepata kura 6,762,224.

https://p.dw.com/p/2i5rO

Rais Uhuru ametoa mwito wa amani na umoja baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais ulioshuhudia kivumbi kikali. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 55 ambaye amekuwa madarakani tangu 2013, ameshinda muhula wa pili wa miaka mitano kwa kujinyakulia asilimia 54.27 ya kura, akifuatiwa na kiongozi wa upinzani Raila Amolo Odinga aliyepata asilimia 44.74, tume ya uchaguzi imesema siku ya Ijumaa. 

Haijabainika wazi ikiwa Odinga na muungano wake wa upinzani NASA utayakubali matokeo hayo, baada ya kudai mapema wiki hii kwamba wadukuzi waliungilia mfumo wa uchaguzi.

Mwandishi:Josephat Charo/dpae/afpe