Uhamiaji haramu- Safari ya mauti
27 Aprili 2015Bahari ya Mediterrenean inayoiunganisha Afrika ya Kaskazini na Ulaya imebadilishwa jina sasa na kuitwa "Bahari ya Mauti" kwani takribani kila siku mamia ya wahamiaji haramu kutoka Afrika na Asia hujaribu kuivuuka bahari hiyo katika jitihada zao wa kuingia barani Ulaya, wanakosema kuwa wanafuatia maisha mazuri. Matokeo yake wengi wao huzama wakiwa mkondoni, kwani wanatumia usafiri usio wa uhakika na wa kimagendo. Idadi ya vifo inazidi kupanda kila uchao.
Kwenye mtiririko huu wa makala, habari na mahijiano, Deutsche Welle inakuletea undani wa safari hizi, maisha ya kabla na baada ya safari kwa wale wanaofanikiwa kuvuuka, sababu halisi za wahamiaji haramu na juhudi zinazochukuliwa na dunia kukomesha safari hizi za mauti. Ungana nasi kila siku mchana kujifunza ukweli halisi.