Ubingwa wa Uhispania kuwaendea Atletico au Barcelona? | Michezo | DW | 12.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ubingwa wa Uhispania kuwaendea Atletico au Barcelona?

Utakuwa ni mpambano wa kufa na kupona, katika siku ya mwisho ya msimu katika ligi kuu ya soka Uhispania, wakati Barcelona watakapowakaribisha Atletico Madrid uwanjani Camp Nou.

Mechi hiyo ndiyo itakayoamua mshindi wa msimu huu wa taji la ligi kuu ya soka Uhispania, baada ya timu zote mbili kutekwa sare katika mechi zao za hapo jana. Ni wazi kuwa Real Madrid hawako tena katika kinyang'anyiro hicho, baada ya kuduwazwa na Celta Vigo kwa kurambishwa magoli mawili bila jawabu.

Atletico walitoka sare ya goli moja kwa moja na Malaga, wakati Elche wakiwateka miamba Barcelona kwa kutofungana goli lolote. Atletico sasa watahitaji tu sare watakapokutana na Barca, lakini kama Barca watapata points tatu, basi wataweza kulihifadhi taji lao kwa sababu watakuwa na points 89 kila mmoja, ila tu Barca watatawazwa mabingwa kwa sababu ya rekodi ya kuzilinganisha timu hizo mbili ambayo hutumiwa kuamua mshindi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-rahman