Ubingwa wa Bundesliga bado kitendawili | Michezo | DW | 29.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ubingwa wa Bundesliga bado kitendawili

Vinara na mabingwa watetezi Bayern Munich waliponea ugenini walipokuwa wakicheza na Nürnberg kwa kutoka sare ya goli moja hapo Jumapili.

Borussia Dortmund wanaoishikilia nafasi ya pili kwenye msimamowakikosa nafasi nzuri ya kukwea hadi kileleni baada ya kufungwa nyumbani kwao Signal Iduna Park magoli 4-2 walipokuwa wakicheza na Schalke 04 katika Revierre derby.

Kwa sasa Bayern wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 71 huku Dortmund wakiwafuata kwa pointi 69.

Bayern lakini wanaonekana kuwa na kibarua kigumu katika mechi tatu zilizosalia kwa kuwa bado hawajacheza na Eintrach Frankfurt pamoja na RB Leipzig wanaoishikilia nafasi ya tatu.

Fußball Bundesliga 31. Spieltag l BVB Dortmund vs FC Schalke 04 l 1:3 Rote Karte für Marco Reus (Imago/M. Müller)

Nahodha wa Dortmund Marco Reus akionyeshwa kadi nyekundu

Dortmund wao wana kibarua dhidi ya Werder Bremen katika mojawapo ya hizo mechi tatu zilizosalia msimu kufikia kikomo. 

DW inapendekeza