1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Kenya yatoa neno kuhusu vyakula vya GMO Kenya

Shisia Wasilwa
29 Novemba 2022

Mahakama Kuu nchini Kenya imesitisha mpango wa serikali wa kuchapisha kwenye gazeti rasmi, uagizaji wa vyakula vilivyokuzwa kwa njia ya kisayansi, GMO hadi kesi itakaposikizwa na kuamuliwa

https://p.dw.com/p/4KDRV
Laborassistent testet GMO Hühnchen
Picha: Elnur/imago images

Maagizo ya Mahakama yametiwa sahihi na jaji Mugure Thande, na hivyo yanaizuia serikali au waziri yeyote kuondoa marufuku ya kuagiza vyakula vinavyokuzwa kwa njia ya kisayansi nchini Kenya.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamni na kundi la wakulima wa kiwango cha chini wanaoshikilia kuwa hatua ya kuagiza vyakula hivyo itaaathiri biashara zao. Serikali ya Kenya imesema hatua ya kuagiza vyakula hivyo imefikiwa kutokana na uhaba wa chakula nchini pamoja na kiangazi ambacho kimewaathiri watu milioni nne, huku majimbo 23 yakiathriwa. Matamshi ya waziri wa viwanda na biashara Moses Kuria yanazidi kuibua hisia kali kutoka kwa viongozi mbali mbali.

soma zaidi:Upinzani wamkosoa Ruto kwa kwa kuruhusu vyakula vilivyokuzwa kisayansi

Kesi hiyo ni ya pili dhidi ya serikali ya Rais William Ruto kuwasilishwa. Kesi ya kwanza dhidi ya vyakula hivyo iliwasilishwa na Paul Mwangi. Aliishtaki serikali kwa kuondoa marufuku dhidi ya vyakula hivyo iliyopitishwa kwenye serikai ya rais Mwai Kibaki.

Wakulima wadai hatua ya serikali imekiuka  sheria

Meismehl GMO Bosnien
Maandiko ya maneno ya vyakula vinavyokuzwa kisayansi GMO Picha: DW

Kikundi cha wakulima wadogo kilichowasiisha kesi hiyo kinadai kuwa hatua ya serikali imekiuka utaratibu wa sheria kwani umma hukuhusishwa kwenye maamuzi. Aidha kikukndi hicho kinadai kuwa vyakula hivyo si bora kwa afya. Baadhi ya viongozi wamemtaka Rais William Ruto kufikiria tena kuhusu uamuzi huo.

soma zaidi:Serikali ya Kenya yabatilisha uamuzi wa kupiga marufuku mbegu za GMO

Vyakula vya GMO vilipigwa marufuku kwenye serikali za Rais Mwai Kibaki mwaka 2012 pamoja na rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Ripoti moja ilihusisha vyakula hivyo na ugonjwa wa saratani.

Serikali ya rais Ruto haijawasilisha kesi ya kupinga kesi dhidi yake, huku Rais Ruto akisema uagizaji wa vyakula hivyo ni njia ya kuangazia uhaba wa chakula nchini pamoja na kiangazi ambacho kinashuhudiwa nchini.

Shisia Wasilwa DW Nairobi