1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Tunisia, Libya na Algeria zakutana kuunda muungano mpya

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Tunisia imefanya mkutano wa kwanza wa ushauri na viongozi wa Algeria na Libya kwa matumaini ya kuanzisha muungano mpya wa eneo la Maghreb.

https://p.dw.com/p/4f5Tz
Wawakilishi wa nchi tatu za Maghreb wakutana
Wawakilishi wa nchi tatu za Maghreb wakutana Picha: Moncef Slimi/DW

Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia, Nabil Ammar, alisema kuwa muungano huo unalenga kuendeleza usalama, utulivu na maendeleo katika nchi hizo tatu. Mkutano huo ulifanyika baada ya viongozi wakuu wa Algeria, Libya na Tunisia kukutana katika mkutano wa kilele wa nishati nchini Algeria mwezi uliopita.

Wakati ulipoitishwa wiki iliyopita, vyombo vya habari vya Morocco vilisema kuwa, Algeria imekuwa na dhamira ya kuunda muungano wa Maghrem dhidi ya Morocco ambayo ni hasimu wake wa kikanda.

Rais wa Algeria Abdelmajid Tebboune alisema mapema mwezi huu kwamba kuundwa kwa muungano huo hakulengi taifa jingine na kwamba mlango uko wazi kwa jirani yake, Morocco.