1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya haki Kenya yamtaka Mfalme Charles aombe msamaha

30 Oktoba 2023

Tume ya Haki za Binadamu nchini Kenya KHRC imemtaka Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza kuiomba radhi Kenya kwa udhalilishaji uliofanywa nchini humo wakati wa ukoloni.

https://p.dw.com/p/4YCDq
Mfalme Charles III kuzuru Kenya kwa siku nne kuanzia Oktoba 31, 2023 na atatembelea miji ya Nairobi na Mombasa.
Mfalme Charles III kuzuru Kenya kwa siku nne kuanzia Oktoba 31, 2023 na atatembelea miji ya Nairobi na Mombasa.Picha: Miguel Medina/AFP/pool/AP/picture alliance

Mfalme Charles na mkewe Camilla hapo Jumanne watakuwa wanaanza ziara ya siku nne katika taifa hilo la Afrika Mashariki, hiyo ikiwa ziara yake ya kwanza kama mfalme katika nchi mwanachama wa Jumuiya ya Madola.

Kulingana na Kasri la Buckingham, Mfalme Charles anatarajiwa kuzungumzia "masuala yaliyoleta uchungu zaidi" katika uhusiani wa kihistoria kati ya Uingereza na Kenya.

Uingereza ilikubali kuwafidia zaidi ya Wakenya elfu 5 waliodhalilishwa na kuteswa wakati wa vita kupigania Uhuru vya Mau Mau, baada ya kesi iliyodumu kwa miaka kadhaa mahakamani.

Uingereza ilikubali kuwalipa fidia ya dola milioni 25.