1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi amteuwa Judith Suminwa kuwa waziri mkuu Kongo

Tatu Karema
1 Aprili 2024

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua waziri wa mipango Judith Suminwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4eK14
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi akihutubia wakati wa kongamano la ushirikiano kati ya Uturuki na mataifa ya Afrika mjini Istanbul nchini Uturuki mnamo Desemba 18, 2021
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix TshisekediPicha: Isa Terli /AA/picture alliance

Suminwa ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo wa waziri mkuu nchini Kongo. Uteuzi wa Suminwa unakamilisha wiki kadhaa  zilizoghubikwa na hali ya sintofahamu kuhusu wadhifa huo.

Suminwa aahidi kuleta maendelea Kongo

Katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, Suminwa amesema kuwa anafahamu kuhusu jukumu kubwa linalomkabili na kuongeza kuwa atafanya kazi kuhakikisha kuwepo kwa amani na maendeleo nchini humo.

Soma pia:Mapigano mapya yazuka mashariki mwa DRCongo katika mji wa Sake

Kuapishwa kwa Tshisekedi kwa muhula wa pili madarakani mnamo mwezi Januari, kulianzisha mchakato wa muda mrefu wa kutafuta muungano wa vyama vingi katika bunge la kitaifa, hatua muhimu kabla ya kuteuliwa kwa waziri mkuu na kuundwa kwa serikali.

Soma pia;Umoja wa Mataifa waonya kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama Mashariki mwa Kongo

Serikali ya nchi hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi zinazojumuisha mgogoro unaozidi kutanuka na mzozo wa kibinadamu katika maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo pamoja na usimamizi wa madini.