1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano mapya yazuka mashariki mwa DRCongo

17 Machi 2024

Mapigano mapya yamezuka hapo jana kati ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 katika mji wa Sake unaopatikana takriban kilometa 20 magharibi mwa mji wa Goma.

https://p.dw.com/p/4dpAD
Mapigano katika mji wa Sake- Mkoa wa Kivu Kaskazini, DRC
Raia wa Kongo wakiyahama makazi yao kufuatia kuzuka kwa mapigano katika mji wa Sake mashariki mwa KongoPicha: Benjamin Kasembe/DW

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo Bintou Keita amesema askari wanane wa kulinda amani wamejeruhiwa kufuatia mapigano hayo yaliyozuka mashariki mwa Kongo baada ya siku kadhaa za utulivu.

Luteni kanali Guillaume Ndjike, msemaji wa jeshi katika jimbo hilo, amevishutumu vikosi vya Rwanda kwa kukilenga kituo cha Umoja wa Mataifa huko Sake wakati wa mapigano hayo.

Soma pia: Marekani inalaani ghasia mashariki mwa DR Kongo

Wiki mbili zilizopita, kundi hilo linaloongozwa na Watutsi la M23 lilianzisha mashambulizi mapya na kuilenga miji kadhaa iliyo karibu na Goma, na hivyo kujizatiti katika maeneo ya kaskazini kama Rutshuru na Masisi.