1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Terzic: Tutajitahidi tuwe tena katika nafasi hii msimu ujao

31 Mei 2023

Dortmund walihitaji ushindi katika mechi yao na Mainz au sare katika mechi ya Bayern na FC Köln ili waweze kulinyakua taji lao la kwanza la Bundesliga tangu mwaka 2012.

https://p.dw.com/p/4RwAJ
Fussball Bundesliga, 34. Spieltag l Borussia Dortmund vs FSV Mainz 05 l Enttäuschung, Edin Terzic
Picha: Moritz Müller/IMAGO

Ila sivyo mambo yalivyokuwa kwani walizuiwa sare ya 2-2 na Mainz 05 huku mshambuliaji wao mahiri Sebastian Haller akikosa mkwaju wa penalti katika mechi hiyo.

Kocha Edin Terzic amehuzunishwa sana na jinsi mambo yalivyokwenda ila hajafa moyo amewaahidi mashabiki wa klabu hiyo kwamba watajitahidi msimu utakapoanza wawe katika kinanyang'anyiro cha ubingwa kwa mara nyengine tena.

Fussball Bundesliga, 34. Spieltag l Borussia Dortmund vs FSV Mainz 05 l Enttäuschung, Edin Terzic
Kocha wa Borussia Dortmund Edin Terzic akitokwa na machozi baada ya mechi dhidi ya Mainz 05Picha: Derix/Beautiful Sports/IMAGO

"Sijui, nahisi hatukustahili kuwa katika hali hii ukizingatia tuliyopitia miezi kumi iliyopita na ukiona imani iliyokuwa si uwanjani tu ila katika mji mzima wa Dortmund, tunahuzunika sana na nafasi tuliyoikosa. tulikuwa karibu sana kulishinda taji," alisema Terzic.