Teknolojia kurahisisha manunuzi ya serikali | Matukio ya Afrika | DW | 03.11.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Teknolojia kurahisisha manunuzi ya serikali

Wajumbe wa mamlaka za manunuzi ya umma Afrika Mashariki wamefanya kongamano nchini Uganda. Wamejadili mada ya kuhusisha teknolojia katika michakato ya matumizi ya fedha za serikali zao pamoja na jumuiya.

Sikiliza sauti 02:51

Mahojiano na Matern Lumbanga

Wajumbe kutoka mamlaka za manunuzi ya umma Afrika Mashariki wamekamilisha kongamano lao la kumi mjini Kampala, Uganda, adhuhuri ya leo ambapo wamejadili mada ya kuhusisha teknolojia katika michakato ya matumizi ya fedha za serikali zao pamoja na jumuiya hiyo. Miongoni mwa hoja zilizoibuka katika mashauriano yao ya siku tatu ilikuwa jinsi teknolojia itakavyorahisha shuguli zao kwa uwazi na wakati huku mienendo ya ufisadi ikipunguzwa. Mwandishi wetu Lubega Emmanuel amezungumza na mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma Tanzania, Balozi Matern Lumbanga, ambaye ameanza kwa kufafanua umuhimu wa kongamano hilo la kila mwaka.
 

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com