1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania yasaini mkataba wa reli wa dola bilioni 2 na China

21 Desemba 2022

Tanzania imetia saini jana mkataba wa dola bilioni 2.2 na kampuni ya China kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya mwisho ya reli inayolenga kuunganisha bandari kuu ya nchi hiyo na majirani zake.

https://p.dw.com/p/4LH41
Slowakei Zug
Picha: Vaclav Salek/CTK Photo/picture alliance

Reli hiyo yenye urefu wa kilometa 2,561 itaunganisha bandari ya Dar es Salaam hadi Mwanza na hatimaye kuelekea Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeshuhudia utiaji saini huo, amesema nchi hiyo inapaswa kukopa kwa ajili ya miundombinu muhimu na miradi mingine ya maendeleo endelevu huku akipuuza ukosoaji kwamba nchi inakabiliwa na mzigo wa madeni.

Bi.Samia ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha mwisho wa reli ya kisasa SGR chenye urefu wa kilomita 506 kutoka Tabora hadi Kigoma utakamilika mwaka 2026, miaka tisa tangu ujenzi wake ulipoanza.