1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki za binadamuAfghanistan

Taliban yawauawa wahalifu wawili mbele ya umma

22 Februari 2024

Serikali ya Taliban imewaua watu wawili mbele ya umma uliokusanyika katika uwanja mmoja kusini mashariki mwa Afghanistan hii leo.

https://p.dw.com/p/4cjbq
Baadhi ya Waafhanistan wakiwa katika picha ya pamoja
Baadhi ya Waafhanistan wakiwa katika picha ya pamojaPicha: Ebrahim NorooziAP/picture alliance

Maelfu ya raia, ikiwa ni pamoja na mwandishi wa shirika la habari la AP walikusanyika kushuhudia matukio hayo yaliyofanywa katika eneo la Ali Lala kwenye jiji la Ghazni. 

Vyombo vya habari kwenye eneo hilo vimeripoti kwamba mahakama kadhaa pamoja na kiongozi wa juu zaidi nchini humo Hibatullah Akhundzada waliagiza watu hao kuuawa kutokana na uhalifu walioufanya.

Soma pia:Taliban yakataa kushiriki mkutano kuhusu Afghanistan

Utawala wa Taliban hata hivyo haukutaka kuzungumzia madai hayo ilipoombwa kufanya hivyo.

Watu hao walifyatuliwa risasi 15, mmoja 8 na mwingine 7, yakiwa ni matukio ya tatu na nne ya wahalifu kuuliwa mbele ya umma tangu Taliban iliporejesha udhibiti mwaka 2021.