1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Takriban raia 11 wameuawa mashariki mwa DR Congo

Zainab Aziz
25 Machi 2024

Takriban watu 11 waliuawa katika mashambulizi mawili yaliyofanywa kwa pamoja karibu na Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4e6MU
Mgogoro wa DR Congo
Watu 11 wauwawa Mashariki mwa Congo Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Mamlaka kwenye eneo hilo imelilaumu kundi la waasi la ADF kwa mashambulizi hayo. Augustin Kapupa, afisa katika eneo la Matembo lililokumbwa na shambulio mojawapo amesema watu sita waliuawa kwenye shambulio la Jumamosi usiku.

Kwa mujibu wa afisa wa serikali mjini Beni Makofi Bukuku mj wa Sayo ni eneo la pili lililoshambuliwa  ambako watu watano waliuawa.

Mwanahabari mashuhuri wa DRC ahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela

Ameliambia shirika la habari la AFP kwamba idadi ya waliouawa katika mji huo wa Sayo bado inaweza kuongezeka, huku waasi wakiwa bado wapo katika eneo hilo.

Jumuiya ya kiraia ya Matembo, imesema wakazi wa eneo hilo katika muda wa wiki tatu zilizopita wamekuwa wakielezea wasiwasi wao kwa jeshi kutokana na kuwepo kwa waasi katika eneo hilo.