1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taiwan yakumbwa na mfululizo wa matetemeko ya ardhi

23 Aprili 2024

Taiwan imekumbwa na mfululizo wa matetemeko ya ardhi ambayo baadhi yalifikia ukubwa wa 6.3 kwenye kipimo cha Richter.

https://p.dw.com/p/4f4Sr
Taiwan | Vikosi vya uokoaji
Vikosi vya Uokoaji vya TaiwanPicha: AP/picture alliance

Mamlaka nchini humo hata hivyo zimesema hakukuwa na uharibifu mkubwa ulioshuhudiwa. Matetemeko zaidi yalisikika maeneo ya jimbo la Hualien na mji mkuu Taipei.

Soma zaidi:Mamia wahamishwa kutoka hifadhi ya taifa baada ya tetemeko Taiwan

Mnamo April 3 mwaka huu, watu 17 walikufa huko Taiwan kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 ambalo pia lilisababisha maporomoko ya udongo na uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu.