1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Waliokwama katika hifadhi ya Taroko, Taiwan waokolewa

7 Aprili 2024

Mamia ya watu wamehamishwa kutoka maeneo ambayo sio salama kwenye hifadhi ya taifa yaTaroko Mashariki mwa Taiwan iliyoathirika vibaya na tetemeko la ardhi, la ukubwa wa 7.2 katika kipimo cha Ritcha.

https://p.dw.com/p/4eVuT
Taiwan
Watu zaidi ya 400 waokolewa kutoka hifadhi ya taifa ya Taroko baada ya tetemeko la ardhi kuliharibu vibaya eneo hilo, TaiwanPicha: Suo Takekuma/Kyodo News/AP/picture alliance

Barabara katika eneo hilo la milima ziliharibiwa kufuatia maporomoko ya ardhi. Hata hivyo maeneo mengine yamejaribu kutengenezwa ili kutoa nafasi ya kuwaokoa watalii na wakaazi waliokwama katika hifadhi hiyo ya taifa. 

Watu wengine 9 waokolewa tetemeko la Taiwan

Jana Jumamosi na leo Jumapili zaidi ya watu 400 waliokwama huko waliokolewa kwa kutumia helikopta na magari.

Tetemeko la ardhi lililotokea  siku ya Jumatano wiki iliyopita lilisababisha mauaji ya watu 13 huku wengine zaidi ya 1,140 wakijeruhiwa.