Syria yakosoa hatua ya kuwapa silaha waaasi | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.06.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Syria yakosoa hatua ya kuwapa silaha waaasi

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Syria Walid al-Moualem amekosoa hatua ya nchi marafiki wa Syria kuwapatia silaha waasi, akisema kuwa hatua hiyo haitasaidia juhudi za mkutano wa amani wa mjini Geniva

Machafuko katika mji mkuu wa syria Damascus

Machafuko katika mji mkuu wa syria Damascus

Hayo amayasema leo hii katika mkutano na wandishi wa habari mjini Damascus akisisitiza hatua hiyo ya nchi za magharibi na za kiarabu kuwapa silaha waasi wa Syria ni hatari kwa mazongumzo ya amani ya mjini geniva na itazidisha muda wa mapigano hayo ya miaka miwili ya Syria.

Walid al-Moualem amesema licha ya ahadi za nchi marafiki wa Syria kuongeza msaada wa silaha kwa wasi wa Syria, lakini wapinzani nchini humo wana matarajio madogo ya kupatikana uzani wa nguvu za kijeshi na serikali ya nchi hiyo.

''Kama wao wanatarajia wanaweza kutengeneza usawa wa nguvu za kijeshi,nafafikiria wanahitaji kusubiri hilo kwa miaka kadhaa'' amesema Walid al-Moualem katika mkutano na wandishi wa habari

Aidha Walid al-Moualem amendelea kuonya kuhusu hatua ya kuwapa msaada wa silaha waasi wa Syria, kunaweza kuchoche ugaidi na kuyapa faid zaidi makundi yenye misimamo mikali ambayo yanafungamana na mtandao wa al Qaeda.

Ameongeza kusema hatua hiyo ya nchi marafiki wa Syria katika mkutano wa mjini Doha Qatar, ni hatari kwa sababu ina lengo la kupanua tatizo la syria kwa kuongeza mauaji na machafuko kwa kuwapa motisha magaidi kuendelea kufanya jinai nchini Syria.

Nchi za kiarabu na za magharibi zasisitiza kusaidiwa wassi

Nchi marafiki wa Syria wakutana Doha

Nchi marafiki wa Syria wakutana Doha

Nchi za magharibi na zile za kiarabu pamoja na Uturuki ambazo zipo nyuma ya upinzani nchini syria, zimesema kuwa hatua ya kuwasaidia silaha waasi ni kwa ajili ya kuleta uzani sawa wa mgogoro wa Syria ambao hadi sasa umeua zaidi ya watu93,000, wengi wao wakiwa raia wa kawaida.

Marekani na Urusi wanapanga kufanya mkutnao wa amni mjini Geniva kati ya utawala wa Rais Bashar Al assadi na wapinzani nchini humo, lakini kuna msuguano wa kidiplomasia unaongezeka.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Syria ameendelea kusisitiza kuwa mazungumzo hayo ya amani ya mjini Geniva hayatamfanya Rais Bashar al assadi kuachia madaraka, bali ni kujadili na kuangalia namna ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Rais Bashar al-Assad anaonekana kuendelea kuikomboa miji muhimu ya karibu na mpaka wa Lebanon, miji ambayo inamsaidia kumpa udhibiti kati ya mji mkuu wa nchi hiyo Damascus na ngome yake kuu katika bahari ya Kati

Mgogoro wa Syria ulianza kama maandamano ya amani kupingi miongo minne ya kutawaliwa na familia ya Assadi, lakini imeibukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo pande zote mbili nchini humo zinashirikisha wapiganaji wa nje.

Mwandishi: Hashimu Gulana REUTERS/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com