Sudan: Maandamano yazaa vuguvugu la kugombea uongozi
Kutokana na msako wa waandamanaji mjini Khartoum, mvutano kati ya raia na wanajeshi uliongezeka. Lakini mvutano huo umemalizika kwa sasa. Ifuatayo ni taarifa ya matukio ya nchini Sudan.
Watu walifungua vipi Swaumu zao katika mwezi wa Ramadhani wakati wa maandamano?
Kwa wiki kadhaa katika mwezi wa Ramadhani, maelfu ya waandamanaji walipiga kambi nje ya wizara ya ulinzi ya Sudan wakitaka kuundwe baraza la mpito ambalo lingewajumusuisha raia kwenye kuamua hatma ya nchi hiyo. Mwanzoni mwa Juni jeshi lilitumia nguvu dhidi ya waandamanaji. Watu kadhaa walikufa na baadhi ya walionusurika waliripoti visa vya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia, na matumizi ya nguvu.
Kwa mapenzi ya nchi yangu
Msako dhidi ya waandamanaji, jeshi liliongeza uwepo wake mabarabarani. Waandamanaji wengi walitabiri kwamba jeshi halitakabidhi madaraka kwa raia. Hali hii ndio waliyoitegemea baada ya kuondolewa madarakani Rais wa muda mrefu, Omar al-Bashir.
Tahadhari
Omar al-Bashir aliitawala Sudan kuanzia 1989 hadi Aprili 2019. Aliwakandamiza wakosoaji wake. Mnamo 1999 alilivunja bunge ili kuendelea kubakia madarakani. Jina lake hata hivyo, litakumbukwa kwa jinsi alivyoushughulikia mgogoro wa Darfur. Askarii wake walitumia nguvu na kusababisha vifo vya maelfu ya watu, Bashir anatuhumuwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Dikteta Bashir akiwa mahakamani
Wasudan wengi walikuwa wakiingojea siku hii kwa muda mrefu - siku ambayo Omar al-Bashir atalazimika kuikabili mahakama. Mnamo Juni 16, alifika mbele ya waendehsa mashtaka, akituhumiwa kwa ufisadi na kumiliki wa fedha za kigeni. Baada ya kung’olewa kwake madarakani, vikosi vya usalama vilipata zaidi ya dola milioni moja za Kimarekani zimeshindiliwa kwenye makasha nyumbani kwake.
Sauti za Wanawake
Wanawake wengi walishiriki kikamilifu katika maandamano hayo, na waliyapa sura mpya ya maandamano hayo. Uwepo wao ulisisitiza madai ya waandamanaji ya kutaka demokrasia na haki sawa. Wakati wa msako wa kikatili uliofanywa na vikosi vya usalama, wanawake wengi waliripoti unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji kama njia iliyotumika kuwanyamazisha.
Malkia wa Wanubi- alama ya mapinduzi
Mwanafunzi wa usanifu Alaa Salah alikua ndiye uso wa mapinduzi. Mpiga picha alimpiga picha hii wakati akiwa mesimama juu ya gari anawahutubia waandamanaji. Picha na video za maandamano kumuhusu ziligonga kwenye mitandao ya kijamii. Mitandaoni anajulikana kama "Kandaka" au malkia wa Wanubi.
Kuungwa mkono kimataifa
Shukrani kwa mitandao ya kijamii, maandamano hayo yalipokelewa kwenye ngazi ya kimataifa na yaliungwa mkono na makundi ya kutetea haki za binadamu pamoja na Wasudan wanaoishi nje ya nchi. Katika taarifa yao, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Umoja wa Ulaya walihimiza kukomeshwa mara moja aina zote za dhuluma dhidi ya raia wa Sudan.