Suarez asema yuko tayari kwa El-Classico | Michezo | DW | 17.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Suarez asema yuko tayari kwa El-Classico

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, anasubiri kwa hamu kukamilisha adhabu yake aliyopewa na FIFA na anasema atakuwa fit kucheza dhidi ya Real Madrid katika mchuano huo wa El-Classico baadaye mwezi huu

Suarez alikabidhiwa tuzo kutoka kwa shujaa wa Liverpool Kenny Dalglish kwa kuwa mfungaji wa mabao mengi msimu uliopita katika ligi Kuu ya England. Mu Uruguay huyo alipachika jumla ya nyavuni magoli 31.

Alipigwa marufuku ya miezi minne na FIFA pamoja na kufungiwa kucheza mechi tisa za kimataifa baada ya kumng'ata beki wa Italia Giorgio Chiellini katika fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

Adhabu hiyo inakamilika Oktoba 24, na huenda akacheza katika uwanja wa Santiago Bernabeu diku itakayofuata kama atachuguliwa na kocha wa Barca Luis Enrique kitu anachokisubiri kwa hamu kubwa. Suarez amesema "kucheza mechi yangu ya kwanza dhidi ya Real Madrid ni kitu kizuri sana. Niko tayari kufana kile kocha atasema. Mchuano wangu wa kwanza na Barcelona katika uwanja wa Bernabeu ni jambo maalum kwa sababu ya utani wa tangu jadi. Lakini nitajaribu tu kufurahia na kujitahidi nikiwa na jezi ya Barcelona. Hicho ndicho ninalenga kufanya".

Mshambuliaji huyo amekuwa akifanya mazoezi makali na wachezaji wenzake wa Barcelona na yuko tayari kushuka dimbani. Alifunga magoli mawili katika ushindi wa Uruguay wa mabao matatu wka sifuri dhidi ya Oman katika mchuano wa kirafiki mapema wiki hii.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu