Suarez ahamia Barcelona kutoka Liverpool | Michezo | DW | 11.07.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Suarez ahamia Barcelona kutoka Liverpool

Barcelona imemsajili mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez kutoka klabu ya Liverpool, licha ya tukio lililozusha gumzo kote duniani la kumng'ata mpinzani wake katika Kombe la Dunia nchini Brazil

Barcelona walikamilisha jana uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 baada ya kuomba radhi kufuatia tukio ambalo alimng'ata begani beki wa Italia Giorgio Chiellini. Magazeti ya Uhispania yalisema Barcelona waliilipa Liverpool kiasi cha euro milioni 81 huku vyombo vya habari Uingereza vikisema kiasi kilichotumiwa kwa usajili huo ni pauni milioni 75.

Suarez alisema katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Liverpool kuwa anasikitia kuihama Liverpool, ili kuanza maisha mapya na changamoto mpya nchini Uhispania. Suarez atazinduliwa uwanjani Camp Nou wiki ijayo atakaposaini mkataba wa miaka mitano.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu