1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Starmer ataka mzozo wa Ukraine usisahauliwe

18 Machi 2026

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer ameikumbusha jumuiya ya kimataifa kutouusahau mzozo wa ukraine, licha ya vita vinavyoendelea vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

https://p.dw.com/p/5AZxC
Uingereza London 2026 | Keir Starmer amkaribisha Rais Volodymyr Zelensky huko Downing Street
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akizungumza na Rais wa ukraine Volodymyr zelensky na kutaka mzozo wa Kyiv usisahaulikePicha: Suzanne Plunkett/AFP

Starmer alisema hayo alipomkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwenye makazi na ofisi yake, kwenye mtaa wa Downing, jijini London na kuongeza kuwa hawapaswi kupoteza mwelekeo kuhusu kinachoendelea Ukraine na hasa msaada wao kwa taifa hilo.

Zelenskyy alimpa Starmer taarifa kuhusu kile kinachoendelea kwenye vita vyake na Urusi, usalama wa nishati, na juhudi zinazoendelea za kidiplomasia na Marekani na Urusi.

Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte pia alijiunga na mkutano huo na kufanya mazungumzo tofauti na Zelenskyy.