1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Spika wa bunge la Cuba yuko ziarani Kenya

Saumu Mwasimba
21 Februari 2024

Spika wa bunge la Cuba Esteban Lazo yuko ziarani mjini Nairobi ambako amekwenda kujua hatma ya madaktari wawili raia wa Cuba waliotekwa nyara nchini Kenya na wanamgambo wa Al Shabab takriban miaka mitano iliyopita.

https://p.dw.com/p/4chus
Wapiganaji wa Al-Shabab wakifanya mazoezi ya kijeshi katika eneo la Lafofe, kusini mwa Mogadishu
Wapiganaji wa Al-Shabab wakifanya mazoezi ya kijeshi katika eneo la Lafofe, kusini mwa MogadishuPicha: Farah Abdi Warsameh/AP/picture alliance

Taarifa iliyotolewa wizara ya mambo ya nje ya Cuba imeeleza kwamba spika wake huyo yuko Kenya ambako atashirikiana na maafisa wa ngazi za juu wa Kenya katika michakato muhimu ya dharura kuhusiana na suala la madaktari hao.

Spika huyo anatafuta ushirikianao na ufafanuzi kuhusu taarifa zilizochapishwa hivi karibuni zilizoonesha kuwepo uwezekano kwamba madaktari hao Assel Harrera Correa na Landy Rodriguez Hernandez wamefariki, japo taarifa hizo hazijathibitishwa.

Kundi la wanamgambo wanaofungamana na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda lilisema kwamba madaktari hao waliuliwa katika shambulio lililofanyika kwenye mji wa Kusini mwa Somalia wa Jilip Februari 15.

Kamandi ya Marekani barani Afrika ilitoa taarifa jana Jumatatu ikithibitisha juu ya shambulio hilo lililofanywa dhidi ya Al-Shabab.