1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Spika wa bunge DRC ajiuzulu

Bruce5 Februari 2021

Spika wa Baraza la Seneti katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alexis Thambwe Mwamba, amewasilisha barua yake ya kujizulu, ikiwa ni katika hatua ya hivi karibuni ya kuwatenga washirika wa rais wa zamani Joseph Kabila. Thambwe amesema hakuna tena hali ya kuaminiana kati yake na maseneta.

https://p.dw.com/p/3oxGv

Hiyo ni baada ya maseneta 64 kati ya 109 kuanzisha mpango wa kupigwa kura ya kutokuwa na imani naye. Kujiuzulu kwake ni tukio la hivi punde kabisa katika msururu wa kuondoka kwa vigogo wa kisiasa kufuatua mvutano wa kimadaraka kati ya wafuasi wa Kabila na wa Rais Felix Tshisekedi, aliyemrithi kiongozi huyo wa muda mrefu Januari 2019. Bruce Amani amezungumza na Byaombe Lubunga, mshauri wa Kabila, kuhusu hayo na kwanza alitaka kusikia maoni yake juu ya Spika Mwamba kujiuzulu.