Snowden afunguliwa mashitaka | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.06.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Snowden afunguliwa mashitaka

Serikali ya Marekani imefungua mashitaka dhidi ya mfanyakazi wa Shirika la Ujasusi la Taifa Edward Snowden. Snowden amekiri kufichua habari za siri kuhusu mipango ya Marekani ya ufuatiliaji kwa vyombo vya habari

A poster supporting Edward Snowden, a former contractor at the National Security Agency (NSA) who leaked revelations of U.S. electronic surveillance, is displayed at Hong Kong's financial Central district June 17, 2013. Snowden reportedly flew to Hong Kong on May 20. He checked out of a luxury hotel on June 10 and his whereabouts remain unknown. Snowden has said he intends to stay in Hong Kong to fight any potential U.S. moves to extradite him. REUTERS/Bobby Yip (CHINA - Tags: POLITICS CRIME LAW SCIENCE TECHNOLOGY)

China USA Internet Edward Snowden Plakat in Hongkong

Chanzo nchini Marekani ambacho hakikutajwa pia kimesema kuwa serikali ya Marekani inapanga kumrejesha nyumbani Snowden kutoka Hong Kong, ambako anaaminika kuwa amejificha. Gazeti la The Washington Post limesema pia kuwa kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani na waendesha mashitaka inamtuhumu Snowden kwa upelelezi, wizi na utoaji wa mali ya serikali. Mashitaka yote yana adhabu ya hadi miaka kumi gerezani.

Kumekuwa na maandamano ya kumuunga mkono Edward Snowden nchini Hong Kong

Kumekuwa na maandamano ya kumuunga mkono Edward Snowden nchini Hong Kong

Kesi hiyo ilifunguliwa mnamo Juni 14, siku tano baada ya jina la Snowden kujitokeza kama mfichuaji wa habari kuhusu mipango mwili ambayo Shirika la Ujasusi NSA lilikusanya data za simu n mtandao wa internet ili kugundua njama za mashambulizi ya kigaidi.

Snowden anaweza kupinga kuhamihwa kwake

Kesi hiyo huenda ikawa sehemu muhimu ya juhudi za serikali ya Marekani kufanikisha uhamisho wa Snowden kutoka Hong Kong, shughuli ambayo huenda ikageuka na kuwa vita vya muda mrefu vya kisheria. Snowden anaweza kupinga uhamisho wake kwa misingi ya kunyanyaswa kisiasa. Kwa ujumla, muafaka wa uhamisho baina ya Marekani na Hong Kong hautakuwa na idhini ya kumhamisha mtu kwa makosa ya kisiasa. Haijakuwa wazi kama Marekani imetuma ombi rasmi kwa Hong Kong kumhamisha Swnoden, wakati nayo Hong Kong ikisalia kimya kuhusiana na suala hilo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Hong Kong Hua Chunying

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Hong Kong Hua Chunying

Sheria ya Upelelezi ni kosa la kisiasa. Serikali ya Obama sasa imetumia sheria hiyo katika kesi nane za uhalifu katika juhudi za kujaribu kutokomeza ufichuaji wa habari za siri. Katika mojawapo ya kesi hizo, Afisa wa Jeshi Bradley Manning alikiri kutuma zaidi ya ripoti za kijeshi laki saba, habari za siri za kidiplomasia na maelezo mengine kwa mtandao wa udukuzi wa Wikileaks. Kesi yake inaendelea katika mahakama ya kijeshi.

Marekani na Hong Kong zina muafaka

Seneta Bill Nelson, mwanachama wa Kamati ya Baraza la Seneti kuhusu huduma za Jeshi ameikaribisha hatua ya kumfungulia mashitaka Snowden. Amesema kosa alilofanya ni la uhaini na hivyo anataraji kuwa serikali ya Hong Kong itaweza kumtia mbaroni na kumkabidhi kwa Marekani.

Marekani na Hong Kong hushirikiana kuhusu masuala ya utekelezaji wa sheria na zina muafaka unaoziwezesha nchi hizo mbili kuwasalimisha wahalifu. Hata hivyo haki za Snowden za kukata rufaa zinaweza kuchelewesha shughuli yoyote ya kutaka kumkabidhi kwa Marekani.

Mafanikio au kushindikana kwa mchakato wa kumhamisha kutalingana na kile mshukiwa atashitakiwa nacho chini ya sheria ya Marekani, na jinsi inavyoambatana na sheria ya Hong Kong chini ya muafaka wa nchi hizo mbili.

Mwandishi. Bruce Amani/AP

Mhariri: Sekione Kitojo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com