Shambulio mjini Baghdad
4 Januari 2009Matangazo
Baghdad:
Watu 40 wameuwawa baada ya bibi mmoja kujiripua karibu na kiunga cha makaburi ya washiya,kaskazini magharibi ya mji mkuu wa Iraq Baghdad.Watu wasiopungua 50 wamejeruhiwa.Shambulio hilo limetokea katika kituo cha karibu na Quba la imam Musa,katika mtaa wa Kadhimiya,wanakoishi waumini wengi wa madhehebu ya shiya.Waumini wengi walikua wakijiandaa katika sehemu hiyo kwaajili ya kuadhimisha siku kuu ya Ashura itakayoanza wiki hii.