Sebastian Vettel asema bado yupo | Michezo | DW | 18.11.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Sebastian Vettel asema bado yupo

Katika mbio za magari ya Formula One, Sebastian Vettel alishinda mkondo wa nane mfululizo msimu huu na kuweka rekodi mpya katika mashindano ya Grand Prix nchini Marekani Jumapili (17.11.2013)

Dereva huyo Mjerumani wa timu ya Red Bull aliipiku rekodi ya awali iliyowekwa na Michael Schumacher ya ushindi mara saba mfululizo katika msimu mmoja iliyowekwa mwaka wa 2004.

Mfaransa Romain Grosjean wa Lotus alikuwa wa pili huku Mark Webber wa Red Bull akifika jukwaani katika nafasi ya tatu. Ushindi wa Vettel haukuwa tu wake wa nane mfululizo, lakini pia wa 12 msimu huu na wa 38 katika taaluma yake ambayo imekuwa na mashindano 119 kufikia sasa. Kama atashinda mkondo wa mwisho msimu huu nchini Brazil Jumapili ijayo, Vettel mwenye umri wa miaka 26 ataifikia rekodi ya Schumacher ya kushinda mikondo 13 katika msimu mmoja alipokuwa na timu ya Ferrari.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters

Mhariri:Yusuf Saumu