1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Santiago:Gerhard Mucke akiri mauaji yaliyokuwa yamefanyika.

24 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG4V

Gazeti moja nchini Chile limemukuu mwanachama wa zamani wa kundi la kijerumani lijulikanalo kama Colonia Dignidad akiungama kwa mauaji ya mwaka 1973 wakati wa utawala wa Pinochet.

Gazeti hilo linalofahamika kama “la Nacion” limesema, Gerhard Mucke aliwaambia majaji waliokuwa wakichunguza kwamba, kiasi cha watu 22 waliuliwa na jeshi la dikteta wa zamani Augusto Pinochet.

Mucke aliekuwa Mlinzi wa mkoloni wa zamani Paul Schäfer alisema, miaka mitano baadae walizifukua maiti hizo na kuzichoma zilizobakia.

Schäfer ambae ni muanzilishi wa chama cha Colonian Dignidad kilichoanzishwa mwaka 1966 na wafuasi wa kijerumani 300, baadae alifungwa kifungo cha miaka 20 kwa kesi ya unyanyasaji wa watoto.