Safari Rally yarejea tena Kenya baada ya miaka 19 | Michezo | DW | 24.06.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Safari Rally yarejea tena Kenya baada ya miaka 19

Kwa mara ya kwanza baada ya kutofanyika kwa miaka 19 mashindano ya mbio za magari maarufu Safari Rally yamerejea tena nchini Kenya.

Mashindano hayo ni raundi ya 6 ya mashindano ya dunia - World Rally Championship - WRC,  na yamewavutia washiriki 58 kutokea kote ulimwenguni.

Muda mfupi baada ya adhuhuri, Rais Uhuru Kenyatta alizindua rasmi mashindano ya mbio za magari ya Safari Rally kwenye uwanja wa ukumbi wa kimataifa wa mikutano, KICC hapa jijini Nairobi.

Kwenye hotuba yake, mlezi wa Safari Rally ambaye pia ni kiongozi wa taifa alizungumzia umuhimu wa mashindano ya Safari Rally katika historia ya Kenya.

Mashindano yenyewe yanatarajiwa kuanza Ijumaa

Kenya ilishiriki kwenye mashindano hayo ya Safari Rally kwa mara ya mwisho mwaka 2002. Baada ya uzinduzi rasmi, magari hayo ya kasi yalielekea eneo la Kasarani kwa mazoezi rasmi kabla ya kuelekea nje ya jiji hadi mji wa Naivasha.

Kenia Coronavirus Uhuru Kenyatta

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Shindano lenyewe limepangwa kuanza siku ya Ijumaa katika taasisi ya mafunzo ya wanyamapori ya KWS iliyoko mjini Naivasha kwenye barabara kuu inayotokea Nairobi kuelekea Nakuru.

Kenya inawakilishwa na Carl Flash Tundo, Hamza Anwar, Jeremy Wahome na McRae Kimathi. Wahome aliye na umri wa miaka 22 na Anwar wa miaka 26 ni baadhi ya madereva wachanga wa Kenya wanaoshiriki chini ya mwamvuli wa madereva nyota wa FIA, ambao ni mpango maalum wa kimataifa wa kusaka, kuelekeza na kukuza vipaji vya chipukizi wa umri wa miaka kati ya 17-26.

Madereva 4 washushwa daraja

Duru zinaeleza kuwa madereva wengine 13 wa Kenya walibwagwa na hawatashiriki kwenye shindano hilo la kimataifa kwasababu za kiufundi. Baada ya vipimo imebainika magari yao hayajatimiza vigezo vya kiufundi vilivyowekwa.

Saudi-Arabien | Rallye Dakar 2021 - Sebastien Loeb und Co-Fahrer Daniel Elena

Mashindano ya magari

Wakati huhuohuo madereva wengine 4 wameshushwa daraja na watashiriki katika mkondo wa 4 wa mashindano ya kitaifa. Jee wakenya wana mtazamo upi kuhusu mashindano hayo ya kihistoria kurejea Kenya? Baadhi niliozungumza nao walikuwa na haya ya kusema.

Carl Flash Tundo ni mshindi mara tano wa Safari Rally na nyota wa shindano la mwaka huu la Africa Rally Championship Equator Rally alivikwa taji la Intercontinental Rally Challenge,IRC, mwaka 2009 na kuwa mkenya wa pekee kuwahi kufikia kilele hicho.Shindano la magari ya kasi la Safari Rally mwaka huu linaanza leo na litakamilika tarehe 27 mwezi huu.