Rwanda yawashtaki watu 25 kwa usaliti wa nchi | Matukio ya Afrika | DW | 03.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Rwanda yawashtaki watu 25 kwa usaliti wa nchi

Watu 25 wameshtakiwa Rwanda kwa kuisaliti serikali pamoja na uhalifu mwingine unaohusiana na madai ya shughuli zao katika kundi la waasi.

Ruanda Kigali Straße Soldat Wahl 2010 (picture alliance/dpa)

Waendesha mashtaka nchini Rwanda wamesema watu 25 wameshtakiwa kwa kuisaliti serikali na uhalifu mwingine unaohusiana na madai ya shughuli zao katika kundi la waasi lililoanzishwa na mpinzani mwenye makao yake nchini Afrika Kusini.

Wanaume hao walifikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi mjini Kigali kwa mara ya kwanza tangu waliporejeshwa nchini humo mwezi Juni kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikokamatwa.

Washukiwa hao ni pamoja na Habibu Mudathiru, aliyekuwa mwanajeshi nchini Rwanda ambaye waendesha mashataka wanasema alikuwa msimamizi wa mafunzo na shughuli za kundi la waasi la Rwanda National Congress (RNC) nchini Congo lililoanzishwa na Kayumba Nyamwasa.

Nyamwasa aliyekuwa mshirika wa rais Paul Kagame, sasa ni mpinzani wa Rwanda mwenye makao yake nchini Afrika Kusini.

Upande wa mashtaka unasema kuwa baadhi ya washukiwa ni raia wa Burundia huku wengine wakiwa raia wa Uganda.