Rwanda kuifadhili Arsenal | Matukio ya Afrika | DW | 28.05.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Rwanda kuifadhili Arsenal

Rwanda imesaini mkataba na klabu ya soka ya Arsenal ambao unajumuisha ufadhili na kujitangaza kitalii kupitia timu ambayo pia inashabikiwa na rais wa nchi hiyo Paul Kagame. Rwanda haijasema ni kiasi gani italipa.

Sikiliza sauti 02:57
Sasa moja kwa moja
dakika (0)

Mahojiano na Mwang'onda Gabriel

Ni makubaliano ya miaka mitatu ambayo yataitangaza nchi hiyo kitalii kufuatia idadi kubwa ya wanyamapori inayoongezeka katika mbuga zake kuanzia faru weusi, simba, pundamilia na hata nyani wa milimani. Hata hivyo, mpango huo wa Kagame umekosolewa na wanaohisi kwamba Rwanda ina matatizo mengi yanayostahili kushughulikiwa kuliko nchi hiyo kuingia mkataba na Arsenal, huku wengine wakiifananisha hatua ya rais huyo ya kujiongezea muda madarakani kuwa sawa na Arsene Wenger aliyekuwa meneja wa klabu hiyo ya Arsenal aliyejiuzulu mwaka huu baada ya kuiongoza kilabu hiyo kwa miaka 22. DW imezungumza na mwanauchumi ambaye pia ni mwanaharakati kutoka Tanzania, Mwang'onda Gabriel.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com