1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto alaumu watendaji wazembe baada ya mripuko wa gesi

Sudi Mnette
3 Februari 2024

Rais wa Kenya William Ruto leo amewalaumu maafisa wa serikali wazemb na wafisadi kwa mripuko mbaya wa gesi wa Nairobi ambao umesababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi 280.

https://p.dw.com/p/4c0k1
Kenia | Gasexplosion in Nairobi
Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Bila ya kutaja jina la anaetuhumiwa na mkasa huo Rais Ruto, amesema maafisa wa serikali walitoa leseni za kujaza gesi katika maeneo ya makazi ya watu wakati ilionekana wazi kuwa ni jambo lisilofaa, lakini kwa sababu ya uzembe na ufisadi walitoa leseni. Aidha aliongeza kwa kusema wanapaswa kufukuzwa kazi na kufunguliwa mashtaka kwa uhalifu ambao wametenda. Lori lililokuwa limebeba mitungi ya gesi liliripuka usiku wa Alhamisi huko Embakasi, wilaya yenye wakazi wengi jijini Nairobi, na kusababisha uharibifu mkubwa na kuwafanya watu kukimbia kuokoa maisha yao.Jana Ijumaa,Taasisi ya Petroli ya Afrika Mashariki ilisema kwamba mripuko huo ulitokea katika "eneo haramu la kujaza na kuhifadhi gesi ambalo mmiliki wake na baadhi ya wateja walitiwa hatiani na kuhukumiwa Mei 2023.