1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rio de Janeiro:: Brazil yapokewa kwa shangwe nyumbani.

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBi6

Shangwe na hoi hoi zinaendelea nchini Brazil baada ya kulitwaa kombe la Amerika, kwa kuwatandika mahasimu wao Argentina mabao 3-0 katika mechi ya fainali jana usiku nchini Venezuela.

Akizungumza na vyombo vya habari, kocha wa Brazil Carlos Dunga alisema,

“Ninataka kusema ushindi huu ni kwa watoto wote kutoka Rwanda, Angola, Israel, Palestina, Brazil , Yugoslavia ya zamani-watoto wenye kuathirika ,na kwa sababu wana moyo mkunjufu, wana mapenzi wametupa moyo kufanya hivyo katika timu yetu Kutokana na hayo ushindi huu ni wao .”

Timu ya Brazil iliwasili Rio de Janeiro na kupokea na mamia kwa maelfu ya mashabiki wa soka nyumbani.