Ribery nje ya Kombe la Dunia | Michezo | DW | 06.06.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ribery nje ya Kombe la Dunia

Matumaini ya Ufaransa katika Kombe la Dunia yamepata pigo kubwa baada ya mchezaji wa pembeni Franck Ribery kujiondoa katika dimba hilo kwa ajili ya jeraha la mgongo

Kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amesema mchezaji huyo nyota amefanyiwa vipimo na sasa kwa bahati mbaya hatoweza kuendelea na mazoezi wala kucheza.

Ribery ambaye amefunga magoli 16 katika mechi 80 za timu ya taifa, alisema hapo awali kabla ya kinyang'anyiro hicho kuwa hili lingekuwa ni Kombe lake la mwisho la Dunia.

Deschamps ametangaza pia kuwa kiungo Clement Grenier hatakuwa katika hali nzuri kuichezea Ufaransa nchini Brazil kutokana na jeraha. Amemwita kikosini kiungo mshambuliaji wa Montpellier Remy Cabella na Morgan Schneiderlin wa Southampton ya Uingereza kuchukua nafasi za Grenier na Robery. Kujiondoa katika dimba hilo kumehitimisha miezi sita ya masaibu ya Ribery, ambaye ni gwiji aliyetamba katika vinyang'anyiro viwili vya Kombe la Dunia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Abdulrahman