Reyes azikwa | Michezo | DW | 03.06.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Reyes azikwa

Jose Antonio Reyes azikwa baada ya jeneza lililobeba mwili wake kupitishwa mitaani katika mji wa Utrera nchini Uhispania

 

Na wakati  huo  huo mamia  ya  waombolezaji  walihudhuria  mazishi nchini Uhispania leo  ya  mchezaji  wa  zamani wa Real Madrid  na arsenal  jose Antonio Reyes, aliyefariki  katika  ajli  ya  gari mwishoni  mwa  juma. Jeneza la Reyes  lililofunikwa  bendera  ya klabu ya  mtotoni mwake  ya  Sevilla, lilipitishwa  mitaani  katika  mji alikozaliwa  wa  Utrera  kabla  ya  kuzikwa.

Fussballer Jose Antonio Reyes (Imago Images/Agencia EFE/A. Martin)

Jose Antonio Reyes

Mchezaji  huyo  wa  zamani  wa  timu  ya  taifa  ya  Uhispania  alifariki Jumamosi  katika  ajali  ya  gari  katika  barabara  kuu  kutoka  Seville kwenda Utrera. Ajali  hiyo  na mripuko wa  moto uliofuatia  pia  umesababisha  kifo  cha  mmoja  wa binamu yake wakati  abiria  mwingine  bado  yuko hospitali  Jumatatu (03.06.2019).

Picha  kutoka  katika  eneo  la  tukio la  ajali  zinaonesha  gari  iliyoungua  moto  ikiwa  imelala juu chini. 

Gazeti  la  kila  siku  la  Diario de Seville  limeripoti  Reyes  alikuwa  anaendesha  kwa  zaidi  ya  kilometa 200 kwa  saa  katika  wakati  wa  ajali  hiyo wakati  gazeti  la  michezo  la  Mundo Deportivo , likinukuu ripoti  ya  polisi, ikisema  alikuwa  anakwenda  mwendo  wa  kilometa 237 kwa  saa.

Fussballer Jose Antonio Reyes (picture-alliance/Cordon Press/A. Alcalde)

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid na Arsenal Jose Antonio Reyes

Alipowasiliana  na  shirika  la  habari  la  AFP, msemaji wa  jeshi  la  pilisi  la  Uhispania  ambalo  linafanya  uchunguzi  wa  ajali  hiyo  alikataa  kutoa  maelezo kuhusu  ripoti  hiyo.