Real Madrid yainyoa Barcelona katika El Classico | Michezo | DW | 28.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Real Madrid yainyoa Barcelona katika El Classico

Barcelona imepoteza mchezo wake wa kwanza Jumamosi, na kuifanya Sevilla kujiunga na Barca kileleni mwa La Liga ikiwa na pointi 22 baada ya ushindi wa mabao 2-1 wa Sevilla dhidi ya Villarreal

Wakati huo huo mchezaji wa kati wa Barcelona Andres Iniesta hataonekana uwanjani kwa karibu wiki tatu baada ya kuumia misuli ya mguu wake wa kulia kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari leo Jumatatu.

Real Madrid sasa iko nafasi ya tatu. Mabingwa Atletico Madrid wameshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Getafe jana Jumapili na iko nafasi ya tano ikiwa na pointi 20, sawa na timu iliyoko nafasi ya nne Valencia , ambayo imeshinda kwa mabao 3-1 nyumbani dhidi ya Elche siku ya Jumamosi.

Chelsea ambayo haijapoteza mchezo hadi sasa katika Premier League nchini England ilikaribia jana kuchupa hadi pointi sita juu ya msimamo wa ligi baada ya michezo tisa lakini Robin van Persie alifunga bao la dakika za mwisho na kuipa Manchester United sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea.

Ushindi wa bao 1-0 wa Southampton dhidi ya Stoke City umeiweka timu hiyo katika nafasi ya pili hadi sasa ikiipiku Manchester City katika nafasi ya tatu. Juventus Turin ina pointi tatu zaidi ya timu inayofuatia katika ligi ya Italia Serie A wakati ilipoishinda Parlemo kwa mabao 2-0. Roma iko nafasi ya pili.

Olympique de Marseille imepoteza mchezo wake wa pili msimu huu wakati Olympique Lyonnais wakiendelea kuwasogelea mahasimu wao wakubwa kwa ushindi wa bao 1-0 . Mabingwa watetezi Paris St. Germain wameishinda Giraundaux Bordeaux kwa mabao 3-0 siku ya Jumamosi.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / ZR / afpe
Mhariri: Yusuf, Saumu