1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo, yuko huru kusafiri

7 Septemba 2023

Utawala wa kijeshi wa Gabon uliomuondoa madarakani aliyekuwa rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba, umesema kiongozi huyo wa zamani yuko huru kuondoka nchini humo.

https://p.dw.com/p/4W3gq
Gabun | Präsident Ali Bongo unter Hausarrest
Picha: TP advisers on behalf of the President's Office/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa yake iliyotolewa kupitia televisheni ya taifa, Rais wa mpito Jenerali Brice Oligui Nguemaamesema Bongo ana uhuru wa kutembea na anaweza hata kusafiri kwenda nje ya nchi kupata matibabu kutokana na hali ya afya yake.

Soma pia: Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo aachiwa huru

Rais huyo aliyepinduliwa, alipata maradhi ya kiharusi Oktoba 2018 yaliyomsababishia ulemavu wa mwili hasa katika kusogeza mguu na mkono wa kulia.

Soma pia: Jumuiya ya ECCAS yaisimamisha uanachama Gabon

Bongo aliyekuwa madarakani kwa miaka 14, amekuwa akishikiliwa nyumbani kwake tangu jeshi la nchi hiyo lilipoipindua serikali yake Agosti 30 muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi uliotajwa na wanamapinduzi hao kuwa wa udanganyifu.