1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo aachiwa huru

Josephat Charo
7 Septemba 2023

Rais wa Gabon aliyepinduliwa Ali Bongo Odimba ameachiwa huru kutoka kifungo cha nyumbani.

https://p.dw.com/p/4W2Rn
Gabun | Präsident Ali Bongo unter Hausarrest
Picha: TP advisers on behalf of the President's Office/AP Photo/picture alliance

Rais wa zamani wa Gabon, Ali Bongo Odimba aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi Agosti 30 ameachiwa huru. Rais wa mpito Jenerali Brice Nguema amesema katika taarifa iliyosomwa katika kituo cha televisheni cha taifa kwamba Bongo yuko huru kuondoka Gabon na kusafiri kwenda nchi za nje akitaka.

Akiisoma taarifa hiyo iliyosainiwa na Nguema, kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi alisema kwa kuzingatia hali yake ya afya Ali Bongo Ondimba ana uhuru wa kutembea na anaweza kusafiri nje ya nchi kama anataka ili kufanya vipimo vyake vya afya. Bongo alipatwa na ugonjwa wa kiarusi mnamo Oktoba 2018 ambao ulimuacha na ulemavu wa mwili hasa matatizo ya kusogeza mguu wake wa kulia na mkono wa kulia.