1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolsonaro miaka 27 jela kwa jaribio la kuipindua serikali

12 Septemba 2025

Majaji wa mahakama kuu Brazil wamemhukumu rais wa zamani Jair Bolsonaro miaka 27 na miezi mitatu jela, baada ya kumkuta na hatia ya kujaribu kufanya mapinduzi ili kuendelea kubakia madarakani.

https://p.dw.com/p/50OSU
Brasília 2025 | Jair Bolsonaro
Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro, akuhumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa jaribio la kuipindua serikaliPicha: Adriano Machado/REUTERS

Bolsonaro, ambae mara zote amekuwa akikataa kuhusika na maovu ya aina yoyote anaweza kuukatia rufaa uamuzi uliotolewa. Kwa sasa yuko katika kifungo cha nyumbani mjini Brasilia.

Majaji wanne kati ya watano waliokuwa wakipitia kesi kesi yake walimkuta na hatia kwa makosa matano, uamuzi utakaozidisha migawanyiko ya kisiasa. 

Makosa hayo ni pamoja na kujaribu kufanya mapinduzi baada ya kushindwa uchaguzi 2022, mipango ya kumuua rais wa sasa Luiz Inácio Lula da Silva, kushiriki katika genge la wahalifu, kujaribu kuvuruga utawala wa sheria pamoja na kuzua vurugu.

Bolsonaro ndio rais wa kwanza wa Brazil kuhukumiwa kwa jaribio la mapinduzi.