1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Kenya atangaza Baraza la Mawaziri

John Juma27 Septemba 2022

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza majina ya baraza lake jipya la mawaziri. Miongoni mwa wale aliowapendekeza ni wapambe wake kisiasa waliomsaidia kwenye kampeni akiwemo Aden Duale ambaye sasa ni waziri wa Ulinzi na Kindiki Kithure ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

https://p.dw.com/p/4HQGs

Wakati huo huo, Rais Ruto ametangaza kujiuzulu kwa aliyekuwa mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti na vilevile kamishna mkuu wa polisi Hillary Mutyambai ambaye Ruto amesema ameomba achukue likizo ya mapema kufuatia hali yake ya afya. John Juma amefanya mazungumzo na mchambuzi wa siasa Barack Muluka kuhusu majina yaliyotajwa na Ruto.