1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Uhuru Kenyata kuhutubia taifa

15 Machi 2017

Macho na masikio ya Wakenya yanaelekezwa katika jengo la Bunge mjini Nairobi, ambako rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta anatarajiwa mchana wa leo kutoa hotuba inayoelezea hali ya taifa.

https://p.dw.com/p/2ZC0Q

Hotuba ambayo kikatiba inatolewa kila mwaka. Mara hii hotuba ya Rais Kenyatta inatolewa mnamo mwaka wa uchaguzi, na ikiwa ni ya mwisho katika muhula wake wa kwanza madarakani wengi wanatazamia kuwa hali hiyo itazingatiwa katika ujumbe atakaoufikisha kwa wananchi. Kutaka kujua hasa matarajio ya wakenya katika hotuba hiyo. Daniel Gakuba kazungumza na Herman Manyora, mchambuzi wa siasa na mhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi, na yafuatayo ni maelezo yake.