1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Tshisekedi awaasa raia kuacha kuuza mali ya taifa lao

Jean Noël Ba-Mweze
16 Januari 2023

Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo ametoa mwito kwa Wakongo kuwa wazalendo zaidi kwa kuepuka biashara haramu au kuuza kiholela mali ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4MFrZ
Deutschland Manching | Goldschatz der Kelten im Museum
Picha: Frank Mächler/dpa/picture alliance

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi ametoa mwito huo wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikisafirisha mzigo wake wa kwanza wa dhahabu kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu, mwishoni mwa wiki kutokana na biashara iliyozingatia haki.

Kupitia Primera Gold DRC, moja ya kampuni zilizoundwa kutokana na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, Kongo imesafirisha kilo 28 za dhahabu iliyochimbwa na wachimbaji wadogo wadogo mkoani Kivu kusini. 

Rais Tshisekedi ameutaja ushirikiano huo kuwa wa faida kwa pande hizo mbili na ambao umekuja kutimiza azma yake ya kuona raslimali za nchi hiyo zinawanufaisha Wakongo.