1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Rais Ruto wa Kenya asisitiza kupeleka polisi nchini Haiti

10 Juni 2024

Rais William Ruto wa Kenya amesema atatuma kikosi cha polisi nchini Haiti katika wiki chache zijazo licha ya changamoto za kimahakama kuuchelewesha mchakato huo.

https://p.dw.com/p/4grmV
Rais William Ruto wa Kenya
Rais William Ruto amesisitiza kwamba atapeleka jeshi la polisi nchini Haiti licha ya vikwazo vya kisheria nchini mwakePicha: Dominika Zarzycka/NurPhoto/picture alliance

Akizungumza wakati wa ziara yake eneo la kati la Kenya, Ruto amesema watu wa Haiti wanangoja, na pengine atapeleka kikosi hicho wiki kadhaa zijazo ili kusaidia juhudi za kurejesha amani katika taifa hilo la Karibia.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limesema litatuma maafisa 1,000 kwa ajili ya misheni hiyo pamoja na wafanyakazi kutoka nchi nyingine kadhaa.

Mnamo mwezi Oktoba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kutumwa kikosi hicho, lakini mnamo mwezi Januari, mahakama ya Kenya ilisema kwamba serikali haikuwa na mamlaka ya kutuma maafisa wa polisi nje ya nchi bila makubaliano ya awali.