Rais Rajoelina adaiwa kukimbilia kusikojulikana
13 Oktoba 2025
Matangazo
Kiongozi wa upinzani nchini Madagascar, Siteny Randrianasoloniaiko amesema rais Andry Rajoelina ameikimbia nchi.
Kiongozi huyo wa upinzani ameliambia shirika la habari la Reuters hivi leo kwamba taarifa za kuondoka nchini, Rajoelina zimaethibitishwa na wafanyakazi wa ofisi ya rais.
Hata hivyo msemaji wa rais hakupatikana mara moja kutowa tamko kuhusu taarifa hiyo, alipotafutwa na shirika la habari la Ufaransa, RFI.
Kiongozi wa upinzani Randrianasoloniaiko amesema raisAndry Rajoelinahajulikani aliko na kwamba bunge linalohodhiwa na upinzani litaanza mchakato wa kumuondowa madarakani.
Rais Rajoelina alitarajiwa baadae leo kulihutubia taifa kufuatia maandamano makubwa ya vijana wanaoungwa mkono na jeshi.