1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndonesia

Rais Mteule wa Indonesia Prabowo Subianto atembelea China

1 Aprili 2024

Rais Mteule wa Indonesia anakutana na Rais wa China kwa mazungumzo ya ngazi ya juu, kiasi miezi mwili tangu Subianto aliposhinda uchaguzi katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi Kusini Mashariki mwa Asia.

https://p.dw.com/p/4eJLM
Rais Mteule wa Indonesia Prabowo Subianto
Rais Mteule wa Indonesia Prabowo SubiantoPicha: Oscar Siagian/Getty Images

Rais Mteule wa Indonesia Prabowo Subianto anakutana na Rais wa China Xi Jinping mjini Beijing hii leo kwa ajili ya mazungumzo ya ngazi ya juu.

Ziara hiyo anaifanya kiasi miezi mwili tangu Subianto aliposhinda uchaguzi katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi Kusini-Mashariki mwa Asia.

Soma pia: Mgombea urais Indonesia kupinga matokeo mahakama ya katiba

Prabowo anaizuru China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping kujadili uhusiano wa pande mbili, licha ya ukweli kwamba Rais huyo mpya ataapishwa mnamo mwezi Oktoba.

China imekuwa nchi ya kwanza ya kigeni kutembelewa na Prabowo kama Rais Mteule kabla ya majirani wa Indonesia katika kanda hiyo, hali inayotilia mkazo, uhusiano wa karibu uliojengwa katika muongo uliyopita chini ya mtangulizi wake Joko Widodo.