1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea urais Indonesia kupinga matokeo mahakamani

Saumu Mwasimba
13 Machi 2024

Aliyegombea urais nchini Indonesia, Anies Baswedan amesema anapanga kufunguwa kesi katika mahakama ya katiba kupinga matokeo ya urais kufuatia uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4dSWa
Indonesien, Jakarta | Anies Baswedan
Mgombea wa urais wa Indonesia Anies Baswedan mara baada ya kupiga kura Picha: Andhika/Detik

Aliyegombea urais nchini Indonesia, Anies Baswedan amesema anapanga kufunguwa kesi katika mahakama ya katiba kupinga matokeo ya urais kufuatia uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita. Anies ambaye alikuwa gavana wa mji mkuu Jarkata amesema anapanga kufunguwa kesi hiyo ya malalamiko baada ya matokeo rasmi kutangazwa ingawa hakutowa ufafanuzi zaidi.Rais wa Indonesia ampongeza mshindi wa uchaguzi Prabowo

Hatua ya mwanasiasa huyo inakuja katika wakati ambapo vyama vinavyomuunga mkono,pamoja na mgombea mwingine wa urais,Ganjar Pranowo,wakijiandaa kuanzisha uchunguzi bungeni,kuhusu mwenendo wa serikali kuelekea siku ya uchaguzi pamoja na madai ya kukiukwa sheria za uchaguzi.

Matokeo yasiyokuwa rasmi yanaonesha waziri wa ulinzi Prabowo Subianto aliyeungwa mkono na rais anayeondoka madarakani,Joko Widodo,alishinda uchaguzi huo uliofanyika Februari 14 kwa takriban asilimia 60. Tume ya uchaguzi ya Indonesia inatarajiwa kutangaza matokeo rasmi March 20.