1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Indonesia ampongeza mshindi wa uchaguzi Prabowo

Bruce Amani
15 Februari 2024

Rais wa Indonesia Joko Widodo amesema amempongeza Waziri wa Ulinzi Prabowo Subianto baada ya matokeo yasiyo rasmi kuonyesha kuwa kamanda huyo wa zamani wa vikosi maalum anaelekea kushinda uchaguzi wa rais.

https://p.dw.com/p/4cQzO
Indonesia | Prabowo Subianto na Gibran Rakabuming Raka R
Picha: Agung Kuncahya B./Xinhua/IMAGO Images

Rais wa Indonesia Joko Widodo amesema amempongeza Waziri wa Ulinzi Prabowo Subianto baada ya matokeo yasiyo rasmi kuonyesha kuwa kamanda huyo wa zamani wa vikosi maalum anaelekea kushinda uchaguzi wa rais wa wiki hii katika duru ya kwanza ya upigaji kura.

Mgombea mwenza wa wa Prabowo ni mtoto wa kiume wa Widodo, Gibran Rakabuming Raka, anayetarajiwa kuwa makamu wa rais mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Soma pia: Widodo ashinda uchaguzi wa urais Indonesia

Prabowo, mwenye umri wa miaka 72, alitangaza kile alichosema ni ushindi kwa Waindonesia wote" mbele ya wafuasi wake jana jioni, baada ya matokeo ya haraka ya mashirika huru ya utafiti wa maoni kuonyesha kuwa ameshinda kwa karibu asilimia 60 ya kura.

Wachambuzi huru wanasema hakukuwepo na dalili za udanganyifu wa kimfumo katika uchaguzi huo.