Putin apata ushindi mkubwa | Habari za Ulimwengu | DW | 03.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Putin apata ushindi mkubwa

MOSCOW.Matokeo ya awali katika uchaguzi wa bunge nchini Urusi, yanaonesha kuwa Chama cha Rais Vladmir Putin cha URP kimepata ushindi wa takriban asilimia 63.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi, wakati karibu nusu ya kura zote zikiwa zimehesabiwa chama hicho kinaongoza huku chama cha kikoministi kikamata nafasi ya pili kwa asilimia 11.5.

Hata hivyo kumekuwa na shutuma kuwa uchaguzi huo wa kuwania viti vya 450 vya bunge la nchi hiyo, hakuwa huru na haki.

Hapo janaKansela Angela Merkel wa Ujerumani aliishutumu serikali ya Putin kwa kuvikandamiza vyama vya upinzani.

Pia alielezea kusikitishwa kwake na kutokuwepo kwa waangalizi kutoka shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya katika uchaguzi huo.

Hata hivyo Kansela Merkel alisisitiza kuwa ni muhimu kudumisha uhusiano mzuri na Urusi kwani nchi hiyo ina mchango muhimu katika suala la mzozo wa mpango wa nuklia wa Iran na majaaliwa ya jimbo la Serbia la Kosovo.

Wadadisi wanasema kuwa ushindi wa Putin katika uchaguzi huo utamuweka kiongozi huyo katika ushawishi mkubwa wakisiasa mwakani wakati atakapong´atuka urais kama katiba inavyomtaka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com