1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Presseschau: Maoni ya Wahariri wa magazeti ya Ujerumani

Zainab Aziz Mhariri: Mohamed Khelef
12 Februari 2020

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumia tena uamuzi wa mwenyekiti wa chama cha CDU Kramp-Karrenbauer kujiuzulu na kutogombea ukansela na kuhusu kuachia ngazi kwa mwenyekiti wa baraza la maaskofu nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/3XeNL
Berlin CDU Pressekonferenz Annegret Kramp-Karrenbauer
Picha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Mhariri wa gazeti la die tageszeitung juu ya uamuzi wa mwenyekiti wa chama cha CDU Kramp-Karrenbauer kujiuzulu wadhifa huo anasema kwamba uamuzi wa Kramp-Karrenbauer maana yake ni kufikia mwisho kwa wanawake kuwa kwenye uongozi wa chama cha CDU baada ya kipindi cha miaka 20. 

Siyo jambo la kushangaza kwamba sasa majina yanayotajwa ya wanaoweza kushika wadhifa wa mwenyekiti wa chama hicho kikuu nchini Ujerumani, ni yale ya wanaume tu. Hata hivyo katika zama hizi za akina Trump, Erdogan na Putin ni vizuri kuwa na kiongozi wa chama kama hicho cha CDU mwenye uwezo unaodhibitika.

Mhariri wa gazeti la Osnabrücker anauliza  jee chama cha CDU kinawakilisha maadili gani na gazet hilo linaeleza kwamba mtazamo wa wastani ndani ya chama hicho ulianza kufifia tangu Angela Merkel alipoikumbatia sera ya chama cha SPD juu ya wakimbizi na pia tangu aanze kumsikiliza mwaharakati wa mazingira GretaThunberg.

Imo mivutano ndani ya chama cha CDU, hata hivyo yeyote atakayechukua nafasi ya Kramp-Karrenbauer atapaswa kuyajenga upya maudhui ya chama. Naye mhariri wa gazeti la Frankfurter Allgemeine anasisitiza kwamba chama cha CDU kinahitaji mtu atakaechukua  hatua  za haraka ili kuleta umoja ndani ya chama.

Mwenyekiti wa baraza la maaskofu nchini Ujerumani Kadinali Reihard Marx
Mwenyekiti wa baraza la maaskofu nchini Ujerumani Kadinali Reihard MarxPicha: picture-alliance/dpa/A. Arnold

Juu ya uamuzi wa mwenyekiti wa baraza la maaskofu la nchini Ujerumani Kadinali Reihard Marx wa kutogombea tena wadhifa huo, mhariri wa gazeti la Süddeutsche anasema uamuzi wa mwenyekiti huyo Kadinali Marx ni pigo kwa kanisa katoliki na kwa nchi nzima. Neno la kadinali huyo limekuwa linasikilizwa  katika jamii hii ambapo maaskofu hawana sauti tena. Wakati wa uongozi wake Kadinali Reinhard Marx alisimama kidete kuyatetea maslahi ya wanyonge, ikiwa pamoja na wakimbizi nchini Ujerumani na pia aliwakilisha mtazamo wa mageuzi ndani ya kanisa.

Mhariri wa gazeti la Köln Stadt-Anzeiger anasema yeyote atakayechukua nafasi ya kadinali Marx atapaswa kuizingatia mitazamo tofauti ndani ya kanisa katoliki nchini Ujerumani. Mhariri anaelezea kwamba wapo maaskofu wanaotaka mageuzi, wapo wale wenye mtazamo wa kihafidhina wasiotaka mabadiliko na wapo wale ambao ni wengi wanaotambua kwamba kanisa katoliki linakaribia kusambaratika nchini Ujerumani na mwenyekiti mpya atapaswa kuyazingatia hayo yote.

Mhariri wa gazeti la dietageszeitung anasema Uturuki imejiweka katika mkondo wa vita na Syria hasa kutokana na kauli ya Rais wa Uturuki RecepTayyip Erdogan ya kutishia kufanya mashambulio zaidi baada ya askari watano wa Uturuki kuuliwa na wengine watano walijeruhiwa katika jimbo la waasi la Idlib, ambapo jeshi la Uturuki lilifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi. Mhariri wa gazeti la die tageszeitung anasema kuongezeka idadi ya askari wa Uturuki wanaouawa kunathibisha hali hiyo.

Mhariri wa gazeti la Die Welt ameandika juu ya mikingamo ya mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka China Ai Wie wei aliyepewa hifadhi ya ukimbizi nchini Ujerumani mnamo mwaka 2015.

Kauli za mwanaharakati huyo juu ya Ujerumani zimezua utata, alitoa kauli juu ya ubaguzi, ufashisti na majikwezo kuhusiana na Ujerumani. Kauli za mwanaharakati huyo zinaonekana kana kwamba hakutaka kuja Ujerumani lakini sasa maerejea tena na kwamba anataka kubakia nchini humu. Mhariri wa gazeti la Die Welt anasema inafaa kutilia maanani kwamba ni kutokana na juhudi za serikali ya Ujerumani kwamba aliweza kuachiwa huru na kuweza kuondoka China.

Vyanzo: Deutsche Zeitungen