Polisi yalaumiwa kutumia nguvu kupindukia kiasi | Habari za Ulimwengu | DW | 19.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Polisi yalaumiwa kutumia nguvu kupindukia kiasi

LONDON: Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu limewakosoa polisi wa Kenya kuhusu hatua zilizochukuliwa wakati wa maandamano ya upinzani ya siku tatu nchini humo.Msemaji wa Amnesty International ametamka kuwa polisi walitumia nguvu kupindukia kiasi,walipowafyatulia risasi waandamanaji.Amesema,serikali ya Kenya inapaswa kufanya uchunguzi ulio huru na pia maafisa waliohusika wabebe dhamana ya tukio hilo.

Si chini ya watu 25 waliuawa wakati wa maandamano ya siku tatu ambayo yalimalizika siku ya Ijumaa. Upande wa upinzani sasa umetangaza mpango wa kususia biashara za matajiri wanaofungamana na serikali ya Kenya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com